MWASUKA SASA AKUTANA NA MAWAKALA WA BIMA ZISIZO ZA MAISHA!!

Kitengo cha Masoko na Huduma kwa wateja cha Shiriki la Bima la Taifa (NIC )2010 Ltd chini ya Mkurugenzi wake wa Masoko na Huduma kwa wateja Aloyce Mwasuka leo kimeendelea na utaratibu wake wa kukutana na mawakala wa kampuni hiyo ambapo leo ilikuwa zamu ya Kitengo cha huduma za Bima zisizo za Maisha.
Kikao cha leo pia kilikuwa ni mwendelezo wa vikao vya kufahamiana zaidi na kupeana mikakati juu ya itendaji wa kazi za shirika hilo katika kipindi hiki ambapo shirika hilo linaelekea kwenye mfumo mpya bora na wa kisasa kiutendaji hasa katika suala zima la kuhudumia wateja.
Vikao hivyo ni kuwapa mwakala mikakati, vifaa na kuwapa mbinu za kupunguza urasimu kazini wakati wa kuwahudumia wateja, lakini pia akasema nitakuwa pamoja nanyi katika taratibu na utendaji wa kazi za kila siku ili kuhakikisha tunafikia malengo tutakayojiwekea.
Makampuni ya wakala yaliyohudhuria kikao hicho kwa upande wa bima zisizo za maisha ni Tanzania One Insurance Agency,Responsive Insurance Agency, Aneto Insurance, Kilimanjaro Agency, Machupa General Spplies, TMN Insurance Agency,Kinyonya Insurance Agency, Kina Insurance Agency,Sair Insurance Agency na nyingine nyingi
Wafanyakazi mbalimbali wa kitengo cha masoko na huduma kwa wateja wakiwa katika mkutano huo.



You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment