MASHUJAA MUSIC BAND WANAKAMUA NEW MSASANI CLUB USIKU HUU!


Mdau wa Fullshangwe usiku huu bendi ya muziki ya Mashujaa iko jukwaani kwenye ukumbi wa Msasani Klabu ikiburudisha mashabiki wake kwa nyimbo zake kabambe ambapo burudani kali inaporomoshwa na wanamuziki mahiri kutoka katika kundi hilo linaloongozwa na mwanamuziki nguli na wa siku nyingi nchini Tanzania Elystone Angai akikung'uta gitaa la sollo huku vimwana bomba kabisa wakionyesha uwezo wao wa kuzungusha viuno jukwaani ni burudani tosha kwa mashabiki waliofika kwenye ukumbi huu kwa ajili ya kushuhudia burudani ya wanavibration Sound sasa Mashujaa misic Band.
Vimwana wa Mashujaa Band wakiwajibika jukwaani kweli muziki ni kazi na si kitu cha kufanyia mchezo kama kweli unataka kuwa kwenye gemu ya muziki huku ukiwaburudisha vyakutosha mashabiki wako.
Waimbaji wa bendi ya Mashujaa wakiwajibika jukwaani katika ukumbi wa msasani klabu jijini Dar es salaam usiku huu kwakweli si mchezo ni burudani tu.

Mamaa Flora Bamboocha hakuwa nyuma akafanya vitu vyake kwa pozi kali kabisa mdau unalionaje hilo.

Rose Masaki aka Twiga naye akala pozi kwa staili ya aina yake hebu licheki mdau.
Sharony Mapozi akiwa amepozi mbele ya Camera ya Fullshangwe kwenye ukumbi wa Msasani club jijini Dar. usiku huu.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

2 comments:

  1. hakuna kujenga


    disminers

  2. Tanzania Imekwisha-Kwa namna hii, Majanga yataendelea-Ajali, etc. hadi siku tutakapoiheshimu miili yetu...Sodoma na Ghomora

Post a Comment