MASHUJAA MUSICA BAND YAENDELEA KUTESA DAR ES SALAAM.

Bendi mpya ya muziki wa dansi nchini MASHUJAA BAND, jana iliendeleza wimbi la Maonyesho katika ukumbi wa Equatol Grill ulipo Temeke Mtoni kwa Azizi Alli ikiwa ni katika Bonanza la kila siku ya Jumapili kuanza saa kumi jioni hadi saa sita usiku.
Katika Onyesho hilo wanamuziki na Wacheza shoo wote nyota wa kundi hilo walikuwapo, ikiwa ni pamoja na Kiongozi wa bendi Aliston Angai, Despino Malaika, Geran Kissa, Masooud USB, Ngosha Mwanamasanja, Jado Fidifosi, Pasia Budansi, Raja Rado, na wengine wengi.
Kwa upande wa Burudani ya Shoo bendi hiyo imezidin kung’ara zaidi kutokana na juhudi za Sharony Mapozi, Neema Mkama, Frida Mwanasuka, Sarafina Shotii,Pendo Bonzo, Merisa Maga, pamoja na Etoo Tisa
Hata hivyo bendi hiyo kwa sasa imewezakufanikisha kupata kumbi mbalimbali za burudani kila siku za jumatano hadi jumapili, ikiwa ndiyo kwanza nyimnbo zake zipo sokoni, na tayari zimeshaanza kuwa na mvuto kwenye stesheni mbalimbali za Radio na Televisheni.
Kwa sasa kila ijumaa bendi hiyo inapatikana New Msasani klabu saa tatu usiku, wakati mipango inafanywa ili kupata ukumbi wa Meeda ulipo Sinza ili utumike kwa siku za jumamosi, jumapili ni katika ukumbi wa Ikweta grill uliopo temeke mtoni.Siku ya jumatano ni katika ukumbi wa Woodland uliopo kwa jimmy kiwalani na Alhamis band hiyo itashuka katika ukumbi wake wa nyumbani wa Mashujaa Pub uliopo vingunguti.
Wengine ni mpiga gitaa, Amosi Ras, Baba , Flora Bambucha, Sarafina Shotii, Sharoni Mapozi, Neema Mkama, Pendo Boza, Frida Etoo Tisa, huku waimbaji wakiwemo Ibrahimu Milinda Nyeusi, Pasia Budansi Bakiza Mambo(Raja), Desipino Malaika, Masoud USB, Edward Anthony MaliKidogo(jadol Feed Force FFU) na Mwanamuziki na rapper wa bendi SIMONG NGOSHA(ngosha masanja) Nyimbo zinazovuma kwa sasa ni ule wa Mwanike ulioimbwa kwa mchanganyiko wa makabila ya Kisukuma na Kihaya, ukiwa umetungwa na Ngosha Mwanamasanja na Moshi wa Sigara uliotungwa na mwanamuziki Pasia Budansi.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment