Wasanii wawili wa Muziki wa bongofleva Joh Makini na Gnako usiku wa kuamkia leo walikuwa na kazi ya ziada kupambana na majambazi ili kuokoa maisha yao na mali zao kwa ujumla . wakati Majambazi hao walipovamia nyumbani kwao maeneo ya Changanyikeni nje kidogo ya jiji la Dar es lamaam ili kupora mali, mtonyaji wa habari hizi anasema majambazi hao walifanikiwa kupora vitu mbalimbali simu za mkononi , Deki, Tv, fedha nyingi tu ambazo idadi yake haikufahamika na vingine vingi.
Dj Choka amesema alipata nafasi yakuongea na Gnako na John Makini ili kujua afya zao kama wamejeruhiwa katika tukio hilo au vipi lakini walisema wako salama na wameelezea kuwa tukio hilo lilikuwa kama vile picha ya Rambo kutokana na jinsi mapambano yalivyoendeshwa kati ya majambazi hao na wasanii hao.
Hata hivyo haikufahamika kama Joh Makini na Gnako wameripoti katika kituo chochote cha polisi kwa ajili ya hatua zaidi za kiupelelezi kuchukuliwa kuhusiana na tukio hilo,Poleni sana ndugu zangu....bora mko salama jambo la msingi ni kumshukuru mungu na nina imani mtachapa kazi na mtafanikiwa kupata vifaa vingine kama kawaida
0 comments:
Post a Comment