MAIMARTHA JESSE NA BEN KINYAIYA KUFANYA VITU VYAO NA TBC1!!

Meneja Uhusiano wa kampuni ya 5 Media Company Maimartha Jesse akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati alipotangaza kuanza kazi kwa kampuni hiyo ambayo inamilikiwa na watangazaji na watengenezaji wa vipindi vya Televisheni leo jijini Dar es salaam.
Maimartha amesema kampuni hiyo tayari imeshaingia mkataba wa mwaka mmoja na televisheni ya TBC 1 kwa ajili ya kurusha kipindi cha Afro Pop kitakachokuwa kikifanya mahojniano na wanamuziki na wanamichezo mbalimbali pamoja na watu maarufu katika nyanja tofauti na kupiga nyimbo za kiafrika
Amesema watangazaji wa kipindi hicho watakuwa ni yeye mwenyewe Maimartha Jesse Ben Kinyaiya huku kauli mbiu ya kampuni hiyo ikiwa ni "Kazi kwanza".
Ameongeza kuwa kazi zingine za kampuni hiyo ni pamoja na kubuni na kuandaa vipindi vya televisheniTV Programs, Kuzalisha Video za aina zote Video Productions, Kutengeneza matangzao ya TV, Radio, Barabarani n.k na Kusimamia Matukio na Ushereheshaji.
Maimartha amesema kampuni hiyo iko tayari kufanya kazi na mtu au kampuni yoyote itakayohitaji huduma ya kampuni ya 5 Media Company mwingine aliyeko katika picha ni Afisa habari mwandamizi wa Idara ya Habari Maelezo Benjamin Sawe.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. Atoe na mawasiliano yake ili tumpe kazi na wengine sisi ni MC hivyo tupate kazi pia kutoka kwake kwa kuwa anaweza kupata kazi lakini wa kufanya hakuna hivi tukichukua nafasi sisi basi kazi zinakwneda na kutimiza ile atha ya KAZI KWANZA

    MAHIKE COMMUNICATION FACILITY
    MC KESSY
    Cell +255 713---
    786---55 40 55
    756---

    kessy@linktanzania.com

Post a Comment