Mkurugenzi Mwanzilishi wa Tunaweza Band ambaye pia ni mkurugezi wa kampuni ya Kusafirisha na kupokea vifurushi CDS Bw. Masoud Wanani akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dar es salaam wakati alipotambulisha bendi hiyo ambayo inaundwa na wanamuziki ambao ni walemavu wa Viungo.bendi hiyo itaanza kupiga kwa pamoja na bendi ya African Stars kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni huku ikiongozwa na mwanamuziki wake anayejulikana kama Pajero, bendi hiyo ina nyimbo kadhaa kama vile Tunaweza, Kuku Mido, Raha Dunia na nyingine nyingi.
Amesema Viongozi wengine ni Rais wa bendi Isihaka Kibena ambaye ametoa mchango mkubwa kwa upande wa vyombo vya muziki ambavyo bendi hiyo inatumia, ameongeza kuwa watu wengi wanafikiri mafanikio yanakuja hivi hivi tu, lakini ni vigumu kwani hata kama utafanya kazi sana kitu kikubwa n amuhimu ni kufanya mambo ambayo hata mungu mwenyewe anayapenda.
Anasema kwa mfano yeye toka alipoanza kuwasaidia walemavu hao mambo yake mengi yanaongezeka mpaka huwa anashangaa kwani akitoa milioni moja leo anajikuta kesho anapata kazi nyingine ambayo inamlipa zaidi kwa hiyo muhimu ni kutoa sadaka na mungu atatuona katika shughuli zetu.
Anasema "Kampuni yangu ya CDS ilikuwa ni ndogo sana wakati nilipokuwa nimeianzisha na ilkikuwa haijulikani kabisa lakini kwa sasa ni moja ya kampuni kubwa nchini zinazofanya kazi ya kusafirisha na kupokea vifurushi hapa nchini kwa hiyo kwa mafanikio hayo najisikia kusaidia zaidi bendi yetu hii ambayo inaundwa na walemavu wa viungo na ngozi"






0 comments:
Post a Comment