KERO ZA MUUNGANO ZAANZA KUTATULIWA!!

Katibu mkuu wa Ofisi ya makamu wa Rais Muungano Ruth H. Mollel akiongea na wana habari leo kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo jijini Dar es salaam wengine ni Mkurugenzi msaidizi muungano Baraka.R Baraka katikati na Martha G. Masuki Afisa Mwandamizi Uchumi Muungano.

Kwa mujibu ya katiba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 sura ya pili ibara ya 47 imempa jukumu makamu wa Rais la kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatilia na kutekeleza siku hadi siku mambo yanayohusu Muungano.
Aidha sheria namba 34 ya mwaka 1994 imempa jukumu lengine Makamu wa Rais la kuratibu ushirikiano katika masuala yasiyo ya Muungano kati ya Serikali hizo mbili,yaani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ,Kwa madhumuni ya kuimarisha na kudumisha Muungano wa Tanzania na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa madhumuni ya kuimarisha na kudumisha Muungano kwa njia ya Amani,Upendo na mshikamano wa watanzania wote.
Mafanikio ambayo yamepatikana mpaka sasa hivi kwa kipindi cha miaka minne cha uongozi wa awamu ya nne ni kwamba ofisi ya makamu Rais kwa niaba ya SMT imefanikiwa kwa pamoja na SMZ kushughulikia vikwazo mbali mbali vinavyohusu Muungano.Kamati ya pamoja ,chini ya Uenyekiti wa Makamu wa Rais imeweza kuzijadili hoja tisa na kati ya hizo hoja tatu zimepatiwa ufumbuzi na kuondolewa katika orodha ya kero za Muungano.Hoja zilizopatiwa ufumbuzi:-

Utekelezaji wa sheria ya haki za ubinaadamu
Utekelezaji wa sheria ya “ Merchant Shipping” katika Jamhuri ya Muungano na uwezo wa Zanzibar kujiunga na “International Maritime Organisation” (IMO)
Uvuvi katika ukanda wa bahari kuu.
Ushirikiano katika serikali hizi mbili sasa umeimarika ,vikao vinafanyika kwa madhumuni ya kubadilisha uzoefu na ujuzi,utaalam,sera na mafunzo katika sekta mbali mbali za kitaifa na kimataaifa.
Katika masuala ya kibiashara ,serikali hizo mbili zinashirikiana sana,wananchi wa Tanzania Bara na Tanzania visiwani wanashirikiana bila ya wasiwasi katika masuala ya kuendesha biashara na maisha yao ya kila siku.
Mafanikio mengine ni kwamba kwa mara ya kwanza Ofisi ya Makamu wa Rais imesajili jarida la Muungano linalojuulikana kwa jina la “Muungano Wetu” lenye lengo la kutoa Elimu kwa Umma juu ya masuala ya Muungano.Jarida hilo litakuwa linatoka mara mbili kwa mwaka na linagawiwa bure kwa taasisi mbali mbali na wananchi.
Pamoja na hayo Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Idara yake ya Muungano kwa Umma kupitia Vyombo vya habari vyote yaani Television na Redio,Majarida na Vipeperushi,semina,makongamano n.k.
CHANGAMOTO
Changamoto inayotukabili hivi sasa ni kwamba baadhi ya wananchi hasa vijana waliozaliwa baada ya Muungano bado hawajapata Elimu ya Kutosha kuhusu Muungano.Kwa hiyo ofisi ya Makamu wa Rais inajizatiti kuwaelimisha wananchi wa pande zote mbili ili waweze kuelewa Muungano wetu kwa kuandaa vipindi kwenye Redio na runinga,kuandika Nakala,kwa kutengeneza vipepeperushi na vijarida.Madhumuni ya kufanya hivyo ni kuondoa mashaka yaliyomo kwa baadhi ya wananchi juu ya uhalali wa Muungano.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment