Jitihada za uokoaji zindelea katika mgodi wa Bulyanhulu

Mgodi wa Bulyanhulu umetoa taarifa ya ajali iliyotokea kati ya saa 8 na saa 9 leo alfajiri, ambapo mwamba uliporomoka katika eneo la kazi lililopo wastan wa mita 900 chini ya ardhi. Mwamba huo uliangukia mashine aina ya Jumbo na kuwabana wafanyakazi watatu.
Kikosi cha uokoaji kilianza kazi mara baada ya tukio, shughuli za uokoaji zimekua zikiendelea kwa mfululizo mpaka sasa. Shughuli za uchimbaji zimesimamishwa ili kupisha jitihada za uokoaji, mpaka hapo zitakapokamilika.
Mgodi tayari umeshafikisha taarifa kwa wanafamilia wa wafanyakazi husika, vile vile taarrifa zimefikishwa kwa vyombo mbali mbali ikiwa ni pamoja na Polisi, na uongozi wa mkoa na wilaya. Mgodi unatumia uwezo wake wote katika jitihada za kuokoa wafanyakazi wake na kuwarudisha salama. Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kadri zinavyopatikana.
Kwa taarifa zaidi;
Teweli K. Teweli
PR & Communications Manager
African Barrick Gold
É +255 (22) 216 4229
+255 (22) 216 4229
+255 767 308 600
+255 767 308 600
* tteweli@barrick.com
www.barrick.com

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment