
Mashabiki na wadau kutoka TBC FC wakifurahia matokeo ya timu yao baada ya kushinda magoli mawili kwa moja dhidi ya Jambo Leo FC katika michuano ya NSSF inayofanyika kwenye viwanja vya TCC Siagara Chang'ombe jijini Dar es salaam, magoli yote mawili ya TBC FC yalifungwa na mshambuliaji machachali na aliyeisumbua ngome ya Jambo Leo FC Hemed Salim wakati lile la Jambo Leo FC limefungwa na mshambuliaji hatari wa timu hiyo ambaye pia ni mkurugenzi Mtendaji wa Jambo Leo Juma Pinto.

Mhariri wa gazeti la Spoti Starehe Masoud Sanani na Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano ya NSSF ambaye pia ni mnazi mkubwa wa timu ya Simba akisoma gazeti wakati wakati wa michuanao ya NSSF inayoendelea kwenye viwanja vya TCC Sigara jijini Dar es salaam, kulia ni mhariri wa gazeti la Habari Leo Joseph Kulangwa na kushoto ni Modest Msangi.

Wadau wa timu ya Jambo Leo Joachim Mushi kushoto na Sam Makila wanaonekana wakifuatilia kwa karibu wakati timu yao ya Jambo leo FC ilipopokea kipigo cha goli mbili kwa moja kutoka kwa TBC FC kwa Taaaabu.
0 comments:
Post a Comment