Uchaguzi wa pili wa bunge nchini Iraq tangu uvamizi wa mwaka wa 2003 umegubikwa na ghasia, huku 24 wakiuwawa katika mashambulizi.
Majengo mawili yaliharibiwa katika mji mkuu na makombora kadhaa yalifyatuliwa kote mjini Baghdad na kwingineko.
Mpaka kati ya Iraq na Iran ulifungwa na maelfu ya wanajeshi kupelekwa, huku magari yakipigwa marufuku kupita barabarani.
Waziri Mkuu Nouri Maliki alitoa wito kwa wapiga kura kujitokeza kwa uwingi, na kusema kushiriki kwao kwa uchaguzi kutasaidia demokrasia.
Takriban wachunguzi wa kimataifa wapatao elfu moja na mia tano watafuatilia uchaguzi huo.
Naye kiongozi mwenye msimamo mkali wa Kishia Muqtada al-Sadr, akizungumza katika nchi jirani ya Iran, aliwahimiza wananchi wa Iraq kupiga kura na kukataa ghasia. http://www.bbcswahili.com/

0 comments:
Post a Comment