AMINA SALIM (MAINA) KAHABA ANAYETIKISA KATIKA FILAMU MPYA YA "POOJA"

Amina Salim (Maina) aliyeigiza kama mkuu wa makahaba katika filamu yake mpya ya Pooja
Mariam Mdeme kushoto aliyeigiza kama (mfanyakazi wa ndani) na Amina Salimu aliyeigiza kama (Kahaba) wakipoozi kwa picha

Msanii maarufu wa Filamu nchini Amina Salim a.k.a Mona Salim emesema tayari ameshaipua filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la (Pooja) filamu ambayo amejinasiobu na kusema ni kali na itafunika sana katika ulingo wa filamu nchini.
Amina amesema filamu hiyo imeshirikisha waigizaji maarufu hapa nchini wakiwemo wanamuziki mbalimbali na imeongowa na waongozaji mahiri wa filamu kama vile Tusday Kiangala na Mwigizaji maarufu anayejulikana kama Dude.
Emesema filamu hiyo imeshirikisha waigizaji kama vile Dr. Cheni, Dude, Dotnata., Mzee Chilo, mtangazaji Dida wa Mchops, Jini Kabula, Mwanamuziki Dully Sykes, Jaquiline Woper, Frola Mvungi Kojaki na mwanamuziki wa African Stars Amigolas wengine ni Maoureen Isabela Mpanda, Steve Nyerere.
Dr. Cheni, Mariam Mdeme na Amina Salim ndiyo wahusika wakuu katika filamu hiyo ambapo inaelezea kuwa Mariam Mdeme ni mwanamke ambaye alichukuliwa kijijini kama mfanyakazi wa ndani nyumbani kwa Dr. Cheni hata hivyo kutokana na kufanya kazi kwa bidii na heshima Dr. Cheni aliamua kumuoa akawa mke wake, lakini baada ya muda alikutana na mkuu wa wanawake Changudoa ambaye ni Amina Salim (Maina) akadanganywa na kujiingiza kwenye biashara ya ukahaba, wizi na kutumia dawa za kulevya, baadae waliachyana na Dr Cheni ambaye baadae aliamua kuoa mwanamke mwingine wakati Mariam Mdeme alipata kichaa na kuombewa na Mzee Chilo ambaye alikuwa ni Mchungaji na baadae akapona.
Filamu hiyo ambayo imetengenezwa na Hatman Production na kupigwa picha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kama vile Makongo Lamada Milenium na maeneo mengine mengi itaingia sokoni sokoni hivi karibuni mara baada ya kukamilisha taratibu zote kuhusiana na kazi hiyo ambayo imeelezwa kuwa itatisha mwaka huu katika anga za Filamu

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment