ULINGO - Tanzania Women Crossparty Platform (TWCP) yaja kwa kasi!!

Mwenyekiti wa Chama kipya cha ULINGO Anna Abdallah ( kakati) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu uzinduzi rasmi wa TANZANIA WOMEN CROSSPARTY PLATFORM (TWCP) hapo kesho uzinduzi utakaofanya na (Mke wa Rais Jakaya Kikwete) Mama Salma Kikwete. Ulingo umeundwa kwaajili ya kuwakutanisha wanawake wa Tanzania wenye itikadi tofauti za kisiasa ili kushinikiza ushiriki wao ndani ya medani za uongozi wa kisiasa. wa vyama vya siasa vyenye Uwakilishi Bungeni ambavyo ni CCM/ UWT, Chadema/Bawacha,CUF,TLP,UDP na TWPG. wengine katika picha (kulia ) Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Wabunge Wanawake Tanzania Grace Kiwelu (kushoto) ni Makamu Mwenyekiti wa UWT Asha Bakari Makame. Picha na Mwanakombo Jumaa-Maelezo.

Mama Anna Abdallah amesema malengo makuu ya ulingo(TWCP) ni uwanja wa kuwaunganisha wanawake wanasiasa katika kujadili mustakabali wa nafasi na ushiriki wa wanawake katika uongozi kisiasa hapa Tanzania
TWCP ni rasilimali muhimu katika kuendeleza masuala ya kijinsia kwenye vyama vya siasa na kuweza kutumia fursa iliyopo kuandaa na kuunganisha nguvu katika kujengeana uwezo wa uongozi na kutafuta suluhisho kwa matatizo na vizingiti vya ushiriki na haki za akina mama katika medani ya siasa
Kushirikisha wanawake wengine bila kikwazo cha itikadi za kichama, kujijengea haki ya kukubalika kisheria na uhalali wa kutambuliwa kitaifa na kamataifa,
Ushiriki ulio sawa katika nyanja zote za maendeleo katika nchi pamoja na vyama vya siasa Tanzania
akimalizia amesema mwelekeo ni kuwezesha sauti za wanawake kwa umoja wao zisikike na kuhakikisha wanawake wanapata usawa kwa kuweka mikakati ya pamoja na kushiriki katika sdiasa ndani ya vyama vyao kwa usawa

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment