Wimbi la ajali za barabarani linazidi kupoteza maisha ya watanzania. Katika kile kinachosadikika kuwa ni matokeo ya mwendo kasi wa dreva wa basi la A.M Coach aina ya Scania lenye namba za usajirui T316 AZR lililokuwa likitokea Arusha kwenda Mwanza jana. Basi hilo lilipata ajali nje kidogo ya Mji wa Nzega na watu zaidi ya 24 kupoteza maisha papo hapo na wengine 56 kuachwa wakiwa majeruhi.
Lakini katika hali ya kushangaza, na kama ilivyo kawaida kwa Mji wa Nzega umeme hukatika takiribani mara 12 kwa siku. Hii ilitokea jana wakati majeruhi wa ajali hii walipofikishwa katika Hospitali ya wilaya ya Nzega wakihitaji huduma zinazotumia nishati ya Umeme . Huwezi amini Hospital ya Wilaya haina Generator! hivyo majeruhi walilazimika kupumzika gizani wakisubiri umeme urejee ili wapate huduma kama za ushonaji na X-rays.
Ni vema tukafikia hatua ya kila hospital ya wilaya kuwa na nishati ya umeme mbadala.
Inasadikiwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo wa kasi uliochangia kushindwa kuhimili kusimamisha basi hilo punde tairi lilipopasuka.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Liberatus Barlow amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na mganga katika hospitali ya wilaya ya Nzega, John Mwombeki amethibitish vifo hivyo. Mungu awapumzishe pema marehemu wote. Amin.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Liberatus Barlow amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na mganga katika hospitali ya wilaya ya Nzega, John Mwombeki amethibitish vifo hivyo. Mungu awapumzishe pema marehemu wote. Amin.
0 comments:
Post a Comment