Zuma atetewa dhidi ya madai ya Uzinzi

Rais Jacob Zuma wa Africa Kusini.

Chama tawala nchini Afrika kusini ANC, kimeteta rais Jacob Zuma dhidi ya madai kuwa alipata mtoto nje ya ndoa na kuwa anahaibisha nchi kwa tabia yake ya uzinzi.
Kwa mujibu wa wakuu wa chama, bwana Zuma hajavunja sheria zozote na kwamba hakuna cha kuaibisha katika uhusiano wa kimapenzi kati ya watu wawili.
Vyama vya upinzani pamoja na vyombo vya habari vimemushutumu Zuma kwa kukiuka maadili pamoja na kutoa mfano mbovu kwa nchi inayokabiliana na ugonjwa hatari wa ukimwi.
Mmoja wa wabunge nchini Kenneth Meshoe amemtaka Zuma kutafuta ushuari nasaha kwa tabia yake kama alivyofanya mcheza golf mashuhuri Tiger Woods.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment