Mkutano wa AU Kukamilika leo Adis Ababa!

Mkutano wa viongozi wa serikali za nchi wanachama wa Muungano wa Afrika unaoendelea mjini Adis Ababa, Ethiopia, unamalizika hii leo huku viongozi hao wakitarajiwa kujadili bajeti ya muungano huo.
Kuna mipango ya kuongeza matumizi ya muungano huo hadi dola millioni mia mbili kila mwaka, lakini nchini wanachama wengi wanalalamika kuwa, kwa sasa wanakabiliwa na changamoto kulipa madeni yao kwa muungano huo wa Afrika.
Mkutano huo pia unatarajiwa kuidhinisha azimio la amani na usalama. Hali ya usalama nchini Somalia pia litajadiliwa wakati wa mkutano huo.
Vile suala ya mataifa kadhaa barani Afrika kujitolea kutoa hifadhi kwa wahanga wa tetemeko la ardhi nchini Haiti huenda likajadiliwa.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment