TWANGA PEPETA KUWASHA MOTO KILI MARATHON!!

Wanenguaji wa bendi ya African Stars wakifanya jukwaani.

Bendi ya muziki wa dansi ya African Stars wana wa Kutwanga na Kupepeta wanajiandaa kutoa burudani kali katika mbio za Kilimanjaro Marathon zinazotarajiwa kufanyika februari 28 mwezi huu siku ya jumapili mkoani Kilimanjaro mbio ambazo hushirikisha wanariadha maarufu kutoka mataifa mbalimbali Afrika, Asia Ulaya na Marekani.
Akizungumzia maandalizi ya Bendi hiyo mratibu wa bendi hiyo Martin Sospeter amesema wamejiweka sawa kutoa burudani kali na nzuri itakayowafanya na wao kuitangaza vyema kwa wageni mbalimbali wanaotarajiwa kushiriki kwenye mbio hizo
Ameongeza kwamba kama unavyoijua bendi African Stars ni bendi maarufu nchini na inayojua kupiga muziki hivyo hapana shaka kwamba mashabiki wa bendi hiyo wa mkoani kilimanjaro na kwingineko kanda ya Kaskazini wawe tayari kuipokea bendi yao na itakata kiu yao mara itakapofika huko na kutoa burudani katika mbio hizo zinazodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya TBL kupitia Kilimanjaro Lager na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania
Wakati huohuo Martin amesema mwanamuziki wa bendi hiyo mwenye sauti nzuri Saleh Kupaza tayari ameshatunga wimbo mmoja ambao hivi karibuni utaanza kupigwa katika maonyesho mbalimbali ili kuutambulisha kwa mashabiki wa bendi hiyo, hakutaka kuutaja wimbo wenyewe lakini amesema ni wimbo mzuri na wanaamini utapokelewa vyema na wapenzi wa bendi hiyo

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment