Timu ya Yanga ya jijini Dar es salaam leo imeikung'uta Timu ya Toto Africa kutoka mkoani Mwanza magoli 6-0 bila huruma katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa kwenye
uwanja wa uhuru.
Pamoja na kwamba huwa mashabiki wanadai kuwa timu hiyo ya Mwanza ni tawi la Yanga.
Yanga iliyokuwa imepania kukomesha mtindo wa timu zisizo na uwezo kujigamba kama ilivyofanaya timu hiyo kuwa haitafungwa kirahisi na yanga imeonyesha kuwa ni Nyanya na kwa mwenendo huo ni dhairi kwamba itashuka daraja kutokana na mwenendo wake katika michezo mbalimbali ya Ligi kuu ya Vodacom ambayo kwa sasa inaelekea kumpata bingwa kutokana na kasi ya timu ya Simba yenye pointi 49.
Walikuwa ni wachezaji wa mabingwa hao watetezi Boniface Ambani aliyepiga magoli 3, Jerison Tegete akiifungia timu yake goli moja huku mshambuliaji wa timu hiyo Shamte ally akipiga magoli 3 mengine langoni mwa Toto Africa na kumaliza kabisa Timu hiyo inayotumia uwanja wa CCM Kirimba jijini Mwanza
Kwa ushindi huo mnono Yanga inafikisha pointi 42 ikiwa ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya Vodacom nyuma ya Vinara wa ligi hiyo Simba wanaoongoza kwa pointi 49 kwa tofauti ya Pointi 7, hata hivyo timu ya simba kama itaweza kushinda michezo yake miwili ijayo itakuwa imefikisha pointi 55 na kujitangazia ubingwa wa ligi hiyo mapema kwani hakuna timu itakayoweza kufikia pointi hizo mara baada ya michezo yao yote.





0 comments:
Post a Comment