Caf yasisitiza wapo sahihi juu ya suala la Togo!!

Rasi wa shirikisho la mpira barani Africa CAF Issa Hayatou.

Shirikisho la Soka barani Afrika (Caf) limesisitiza kuwa sahihi kuifungia Togo kushiriki mashindano mawili ya Kombe la Mataifa ya Afrika, licha ya kushutumiwa kutokana na uamuzi huo.
Caf limepuuzilia mbali kile ilichokiita "kampeni za nyombo vya habari zenye lengo la kuharibu sifa nzuri ya soka barani Afrika."
Togo imefungiwa kushiriki mashindano mawili yajayo na pia imepigwa faini ya dola 50,000 kwa kujitoa katika mashindano yaliyofanyika Angola.
Walijitoa kutokana na maagizo ya serikali ya Togo baada ya basi lao kushambuliwa kwa risasi na watu wawili waliokuwemo katika msafara wa timu hiyo kuuawa na wengine saba kujeruhiwa.
Caf imesema wachezaji wa Togo walikuwa tayari kuendelea na mashindano hayo na hivyo wamechukulia uamuzi wa kujitoa ulikuwa ni wa serikali kuingilia.
Uamuzi huo wa Caf ulishutumiwa na serikali, wacheza soka na mashabiki wa mchezo huo, na maandamano yalifanyika mjini Lome kupinga kufungiwa huko.
Lakini baada ya kamati kuu kukutana mjini Lubumbashi, Caf imesisitiza uamuzi wake wa kuifungia Togo unakubalika na kanuni zake.www.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment