Akielezea zaidi katika Sanaa Press Talk hiyo, Katibu Mtendaji huyo wa BASATA Ghonche Materego amesema Moja ya majukumu yake ni kufufua na kuhimiza maendeleo ya sanaa Tanzania, kufanya utafiti juu ya masuala ya sanaa pamoja na kutoa ushauri kwa wasanii wa fani mbalimbali hapa nchini.
Amesema wajibu mwingine walionao BASATA ni kuwaendeleza wasanii kitaalamu ambapo wamekuwa wakitoa mafunzo kwa wasanii mbalimbali. Pia Amesema kuwa BASATA inawajibu wa kuwahamasisha wasanii kushiriki katika maonyesho mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
Akijibu hoja za waandishi Ghonche amesema BASATA wamekuwa na mikakati mingi hivi sasa juu ya kuendeleza fani ya sanaa na Utamaduni hapa Tanzania na kwamba wanamejipanga vyema kutoa mafunzo kwa wasanii wa mikoani na wameanadaa Database ya wasanii wote nchini.





0 comments:
Post a Comment