RAIS KIKWETE AMEMTEUA ALOYCE MWAMANGA KUWA MWENYEKITI WA BARAZA LA TAASISI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA.

Katibu mkuu wa wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dkt. Florens Turuka.

Na Veronica Kazimoto – MAELEZO.Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mhandisi Aloyce Mwamanga kuwa mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Sayansi na Teknolojia mkoa wa mbeya utakaodumu kwa muda wa miaka mitatu.
Taarifa iliyotolewa na Katibu mkuu wa wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dkt. Florens Turuka imemwelezea Mhandisi Aloyce kuwa ni Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya PEMACO BEVI Limited na ni Raisi wa TCCIA.
Wakati huo huo waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa. Peter Msolla amewateua wajumbe tisa kuwa wajumbe wa Baraza hilo laTaasisi ya Sayansi na Teknolojia.Wajumbe hao ni Bwana Suleiman Mmwiri kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Bwana Ignatus Herman kutoka Chuo cha teknolojia ya uhandisi cha Mtakatifu Joseph, Profesa Evelyn Mbede kutoka Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia na Bibi Monica Mbelle kutoka VETA kanda ya Kusini.Wengine ni Mhandisi Asantiel Elias kutoka kampuni ya saruji mbeya,
Bibi Margaret Mgaya kutoka Taasisi ya kilimo uyole, Prof. Joseph Msambichaka kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Mbeya, Dkt Lusajo Minga kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Mbeya na Venance Mwakosya kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Mbeya.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

2 comments:

  1. Pongezi Dr. Turuka, tunakutakia mafanikio katika kutekeleza majukumu yako. Pia mzee Bukuku hongera kwa kuinua quality za picha katika blog hii.

  2. Samahani bro John, Pongezi zangu zinakwenda kwa Eng. Aloyce Mwamanga kwa kuteuliwa kwake na tunamtakia kila la heri. (mkono uliteleza na kuweka jina la Dk Turuka). Mdau wa sayansi UDSM.

Post a Comment