Nemanja Vidic kutocheza na AC Milan!

Nemanja Vidic hatocheza mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano kwa timu 16 zinazowania ubingwa wa Ulaya ambapo Manchester United watakwaruzana na AC Milan.
Mlinzi huyo raia wa Serbian hajacheza mchezo wowote mwaka huu wa 2010 kutokana na maumivu ya mishipa ya mguu na hajasafiri na timu yake kwenda Italia.
Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson kwa sasa ni lazima aamue iwapo atamtumia Jonny Evans au Wes Brown kuungana na Rio Ferdinand katika safu ya ulinzi wa kati.
Ryan Giggs pia hatocheza mchezo huo wa siku ya Jumanne baada ya kuvunjika mkono katika mpambano dhidi ya Aston Villa na Anderson pia hayupo katika kikosi cha Manchester United.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment