MWANDOSYA ATAKA WANAFUNZI WA KIBITI WAWE WADADISI!


NA MAGRETH KINABO – MAELEZO

WANAFUNZI wa shule ya sekondari wa Kibiti iliyoko wilayani Rufiji, mkoa wa Pwani wameshauriwa kuwa wadadisi na wabunifu ili waweze kushindana na vijana wengine duniani hususan katika kipindi hiki cha utandawazi Aidha wanafunzi hao waliaaswa kuachwa kutanguliza fedha na mali katika maisha yao, badala yake watoe kipaumbele kwenye masula ya elimu kwea kuwa ni kitu chenye thamani duniani. Kauli hiyo ilitolewa juzi na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Mark Mwandosya wakati alipotembelea shule kwa madhumuni ya kungalia mfumo wa maji ili kuwawezesha kupata maji ya uhakikika na yakutosheleza. “Nimekuja kuwapa motisha ya kuweza kusoma zaidi, lakini pia ningependa kuwa changamoto ninyi kama vijana ili mwuweze kuishi maisha bora ni lazima muwe wadadisi na kuuliza maswali mnapojadiliana masuala ya kimasomo na mengineo. Mnatakiwa kudadasi mpaka mtakapopata uthibitisho , si kukubali kila kitu,” alisema Profesa Mwandosya. Profesa Mwandosya aliwataka wanafunzi hao,wasiwaogope vijana wengine duniani na kuwaona wao ndio wanaweza kuwa wabunifu na wagunduzi wa mambo mbalimbali kwani Mungu akampa kila mtu hata wao wanaweza kinachotakiwa ni kutokata tamaa. “Mchukia kunyanyaswa kiakili mshindane na wenzenu duniani kwa kuwa wabunifu.Ni lazima mpambane nao na kuonyesha kuwa mnaweza,”alisisitiza. Awali akizungumzia kuhusu hali ya maji shuleni hapo, Makamu wa Mkuu wa Shule, Athuman Mbonde alisema hayatoshelezi na yaliyopo yana chumvi. Waziri Mwandosya alimwagiza Mhandisi ambaye ni Msimamizi wa mradi wa maji wa Kibiti, Romanus Mwanying’o kutoka Shirika la Majisafi na Majitaka Dares Salaam(DAWASA) kuangalia mfumo wa maji shuleni hapo ili kuwahakikisha yanafika na kutosheleza, kupitia mradi wa Kibiti, ikiwemo kuwajengea tanki kubwa la maji. Alilitaka pia liweke mfumo wa kuvuna maji ya mvua huku akisisitiza kwamba anataka shule ziwe mfano bora wa uvunaji wa maji ya mvua.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment