Timu ya Simba ya jijini Dar es salaam leo imefanikiwa kufikisha pointi 49 katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa kwenye uwanja wa Uhuru baada ya kuifunga timu ya Moro United na kujiweka sawa kwa kuukaribia ubingwa wa ligi hiyo 2010/0211.
Katika mchezo wa leo simba walitawala karibu vipindi vyote vya mchezo huo na katika kuthibitisha hilo kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo simba walikuwa tayari wameshajipatia magoli matatu ambayo yaligungwa na wachezaji wake Ulimboka Mkwakingwe 1, Nico Nyagawa 1 Ramadhan Chombo Redondo goli 1 hivyo kwenda mapumziko wakiongoza kwa magoli matatu.Katika kipindi cha pili simba iliongeza tena goli la nne kupitia kwa mchezaji wake Juma Jabu hivyo kufanya timu hiyo itoke uwanjani ikiwa na karamu ya magoli 4-1 dhidi ya Moro unitedi ambayo ilipata goli la kufutia machozi kutokana Kevin Yondani beki wa simba kujifunga mwenyewe baada ya kubabatizwa mpira na washambuliaji wa timu ya Moro United.
Kwa ushindi huo ni dhahiri kwamba Simba haikamatiki tena katika ligi hii ya Vodacom kwa imebakiza michezo miwili tu ili iweze kutangaza ubingwa kabla ya ligi hiyo kumalizika, timu ambayo inaikaribia simba kwa mbali ni Yanga ambayo kwa sasa imefikisha pointi 39 ikiwa ni tofauti ya pointi 10.




0 comments:
Post a Comment