Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Shirika la Synavate Tanzania Jane Mahela(kushoto) akijibu maswali ya waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam juu ya matokeo ya utafiti wa hali ya demokrasia ambao Rais Kikwete aliiogoza kwa kupata asilimia 75 ya wahojiwa kuwa watamchagua tena katika uchaguzi ujao. Kulia ni Meneja wa Utafiti wa Vyombo vya Habari na Umma kutoka Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Synovate Tanzania Abdallah Gunda .
Picha, habari na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dar
Na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dar es salaam
Asilimia 75 ya watanzania waliohojiwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali linajihusisha na utafiti wa masuala ya siasa, uchumi na kijamii wameonyesha kuwa wangependa Rais Jakaya Mrisho Kikwete andelelee kuongoza Tanzania mara baada ya uchaguzi Mkuu mwisho mwa mwaka huu.
Hatua hiyo inafuatia watanzania 2000 waliohojiwa kutoka sehemu mbalimbali kumkubali kuwa Rais Kikwete anastahili kuchaguliwa tena kuwa Kiongozi Mkuu wa Tanzania.
Takwimu hizo zilitolewa jana jijini Dar es salaam na Meneja wa Utafiti wa Vyombo vya Habari na Umma kutoka Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Synovate Tanzania Abdallah Gunda alipokuwa anatoa matokeo ya utafiti wa hali ya demokrasia hapa nchini.
Alisema kuwa asilimia hizo ni zaidi ya theluthi mbili ya Watanzania ambao walihojiwa kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Katika utafiti huo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alipata asilimia 10 wakati Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi alipata asilimia 9 .
Gunda aliongeza kuwa Mwenyekiti wa United Democratic Party (UDP) , Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe na Dkt Salim Ahmed Salim walipa asilimia moja kwa kila mmoja wao ya Watanzania wenye uwezo kupiga kura wakipenda kuwa wanafaa kuwa Rais.
Meneja huyo alisema kuwa katika utafiti wao asilimia mbili ya wahoojiwa wote walisema kuwa wasingependa kueleza nani wangependa awe Rais wakati asilimia mbili nyingine hawajui wa kumchagua.
Aidha katika utafiti huo Chama cha Mapinduzi kilioneka kuwa watu wengi walio karibu nacho kwa kuapa asilimia 70, CHADEMA asilimia 17, CUF asilimia 9, NCCR-Mageuzi kuwa na asilimia 2 huku TLP na UDP zikiwa na asilimia moja kila kimoja.






0 comments:
Post a Comment