PAPII KOCHA ATUMA BARUA TOKA GEREZANI AKIOMBA ASAIDIWE KUIFIKISHA KWA MH.RAIS JAKAYA!!!



KUTOKANA NA ITIFAKI NA KAZI NYINGI ZA RAISI NI VIGUMU KWA MIMI KUONANA NAE ILI NIMPE BARUA HII.
HIVYO WAKATI NAENDELEA KUMTAFUTA NIMEONA NIICHAPE KATIKA BLOG HII HUENDA LABDA WATU WAKE WA KARIBU WANAWEZA KUIONA NA KUMFIKISHIA TAARIFA HIZI..

BARUA YENYEWE INASOMEKA KAMA IFUATATAVYO:

MF/NA: 836'04 Johnson Nguza (Papii Kocha)
Gereza Kuu Ukonga
S.L.P 9091
Dar es Salaam

Mh. Rais Jamuhuri ya Muungano Tanzania

YAH: MAOMBI YA KUPEWA MSAADA (MSAMAHA) WA KUFUTIWA ADHABU YA KIFUNGO NILIYOPEWA NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU.

Husika na somo hilo hapo juu. Mimi ni mfungwa katika gereza kuu Ukonga.
Kwa heshma na taadhima na kwa kutambua utu na huruma yako ya ki MUNGU ulionayo dhidi ya binadamu wenzako pamoja na mamlaka uliokabidhiwa na jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Naanguka na kushika miguu yako mitukufu muheshimiwa rais.
Na kuomba msaada (msamaha) kwako muheshimiwa rais
Kwa njia hii ya maandishi kusudi niweze kuondolewa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani, niliyohukumiwa na mahakama tajwa hapo juu.

Mh.Rais mimi nimefungwa nikiwa bado kijana mwenye umri mdogo. Mpaka sasa natambua wazi hatima pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono yako mitukufu Mh. Rais.

Naomba huruma yako muheshimiwa Rais maana mimi ni mtoto wako ninaehitaji huruma yako wewe mzazi.
Natumaini kauli yako ya mwisho ndio itakayoleta pumzi ya uhai nafsini mwangu

Nakutakia kazi njema, afya njema na maisha marefu.
Mungu akubariki

Wako mtiifu
NO:836'04
JOHNSON NGUZA (PAPII KOCHA)

Na huo ndio mwisho wa barua alionitumia Papii ili imfikie Mh. Rais

KWA HISANI YA BINTI MACHOZI,MANKA KWA HABARI ZAIDI TEMEBELEA

www.ladyjaydee.blogspot.com.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment