Msanii mpya wa mahadhi ya muziki wa ZOUK anayekuja juu kwa kasi ya ajabu zaidi ya kimbunga cha TSUNAMI,ni zao jipya kutoka Nyanda Za Juu Kusini nazungumzia wilaya ya Njombe ndani ya mkoa wa IRINGA Msanii huyu anajulikana kwa jina la kisanii AMANIWETU jina lake halisi ni AMANI SAID KILLO,anaingia kwenye ulingo wa Zouk akijitambulisha na wimbo wake mpya uitwao 'MAPENZI NI ZAWADI' ikiwa ndio maandalizi ya Album yake ya kwanza itakayokwenda kwa jina la MOYO FICHO LA SIRI.
Msanii huyo amesharekodi nyimbo nne katika studio ya SOUND POWER chini ya Producer B Jayzee(THE PROVIDER) studio hiyo ipo Njombe mjini, kazi ambazo amesharekodi ni pamoja naMAPENZI NI ZAWADI,RAFIKI,MOYO FICHO LA SIRI na WAUZA SURA na kazi nyingine mpya inayopikwa jikoni kwasasa inaitwa NIMEMPATA,Hivyo anaomba wapenzi wa muziki wa Zouk wakae tayari kwani mwanzoni mwa mwaka 2010 album yake itakuwa sokoni





0 comments:
Post a Comment