
Hizi ni picha za shujaa Elly Gerald Minja, mwanamichezo mwenye uzoefu wa kupanda Mlima wa Kilimanjaro mara baada ya kuifikisha Bendera ya taifa kwenye kilele cha mlima huo mrefu kuliko yote barani Afrika juzi Jumamosi, ikiwa ni katika kuhitimisha mbio za Bia ya Kilimanjaro zilizobeba kampeni ya "Fikisha Tanzania Katika Hatua ya Juu" ikishirikisha wamariadha nyota zaidi ya 70 waliokimbiza bendera kwa zaidi ya kilomita 567 kwa siku tano kuanzia Dar es Salaam hadi Marangu, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Elly Gerald Minja akiwa pamoja na wenzake kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro mara baada ya kufikisha bendera ya Taifa kileleni hapo.
0 comments:
Post a Comment