
Akizungumzia wiki ya mitindo mwaka huu iliyopewa jina la (Swahili Fashion Week)muasisi na muandaaji wa tamasha hilo Mustafa Hassanali alisema kuwa amefurahishwa sana na bunifu mwaka huu na onyesho hilo na anategemea kuandaa onyesho lililo bora zaidi mwakani.
“Nimefurahishwa sana na sapoti tuliyopata kwa wiki ya Mitindo ya Kiswahili, tumekuwa na siku tatu za maonyesho ya mavazi tukiwa na ukumbi uliyojaa watu. Napenda kuwashukuru sana wote waliowezesha kufanikisha maonyesho ya mwaka huu. Napenda kuwashukuru wabunifu wote walioshiriki na wanamitindo walifanya kazi yao vizuri jukwaani. Mwaka huu tumekuwa na wabunifu wazuri na onyesho zuri zaidi na nina shauku kubwa kuandaa Wiki ya mitindo ya Kiswahili mwaka ujao, aliongeza Hassanali.
Katika siku tatu za maonyesho hayo ya mavazi zilizojumuisha wabunifu kutoka ndani na nje ya nchi, pia kulikuwa na onyesho la mabadiliko ya hali ya hewa na tuzo ya mbunifu mpya ya WAPI vilivyodhaminiwa na British Council Tanzania.
Katika tuzo za mbunifu mpya za WAPI , nafasi ya kwanza ilichukuliwa na 2jenge Afrika Matalay, while second place was taken by Kim Dean and third prize went to Diana Hinji.
Siku ya mwisho ya maonyesho hayo ya mavazi pia kulikuwa na tuzo nyingine kama mgeni mualikwa aliyependeza zaidi ambaye alipata malazi ya bure kutoka nyumba ya Swahili Fashion 2009 Southern Sun Hotel na mshindi alikuwa Caroline ambaye ni mwandishi wa magazeti ya Tanzania Standard.
Tuzo nyingine ilikuwa ni ya mwanamitindo bora wa Wiki ya Mitindo ya Kiswahili 2009 ambayo ilichukuliwa na Victoria Martin kwa kuwa mwanamitindo aliyefanya kazi ya visuri kuliko wote.
Katika wiki hiyo ya mitindo, wabunifu wote walipata mafunzo kutoka kwa walimu wa chuo cha ubunifu Munich nchini Ujerumani kupitia warsha ya siku tatu iliyodhaminiwa na Goethe-Institue Tanzania.
Wabunifu walioshiriki katika wiki ya mitindo ya Kiswahili mwaka huu ni pamoja na Manju Msitta, Ailinda Sawe, Farouque Abdela, na Tanzania Mitindo house na wabunifu wageni watakuwa ni Dorothy Lubega wa Uganda na Vaishali Morjaria kutoka Kenya walioonyesha ubunifu wao siku ya tarehe 4 mwezi huu.
Siku ya Alhamisi tarehe 5 Novemba ilianza kwa onyesho la mabadiliko ya hali ya hewa linalodhaminiwa na British Council, likafuatiwa na maonyesho ya mavazi kutoka kwa Farha Naaz, Kemi Kalikawe, Virginia Njumba na Christine Mhando kutoka Tanzania na Vera Vee wa Kenya na Adelia na Sheila Tique wa Msumbiji.
Siku ya Ijumaa iliaanza kwa wabunifu waliokuwa wanawania tuzo ya mbunifu mpya ya WAPI iliyodhaminiwa na British Council ikafuatiwa na maonyesho mavazi kutoka kwa Khadija Mwanamboka, Zamda George, Robi Morro na Fatma Amour kutoka Tanzania na John Kaveke kutoka Kenya na kumaliziwa na mmoja wa wabunifu maarufu barani Afrika David Tlale wa Afrika ya Kusini.
Maonyesho ya Swahili Fashion Week mwaka huu yaliletwa kwa ushirikiano na kampuni za Vodacom Tanzania na ZTE na malazi ya wageni wa SFW kutolewa na Southern Sun Hotel.





0 comments:
Post a Comment