TUNAWAJALI GROUP KUANDAA KONGAMANO LA KUPUNGUZA AJALI ZA BARABARANI!!

Mwenyekiti wa Bw. Abeid Chembe kulia akizungumzia kongamano la kupunguza ajali za barabarani katika mkutano na wanahabari leo
AmesemaTunawajali Group kwa kudhaminiwa na Sameer Africa Tanzania Ltd (YANA) wameandaa kongamno la utafiti wa vyanzo vya ajali za barabarani Tanzania ili kuitikia mwito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete kwa jamii ambapo alisisitiza matumizi mazuri ya barabara,
hasa zilizojengwa na zinazojengwa kwa kiwango cha lami huku akiomba mwendo kasi wa mabasi na magari mengine uachwe na kuwepo na milango ya dharura katika mabasi na watu waache kuvamia na mambo mengine mengi ambayo yamekuwa yakipelekea kutokea kwa ajali barabarani
Bw. Abeid Chembe amesema wamewafuata wadau mbalimbali kama vile makampuni ya usafirishaji, yanayouza magari, matairi chuo cha usafishaji na wengine wengi ili kuchangia na kufanikisha kongamano hilo ambalo maandalizi yake yanaendelea na tarehe ya kufanyika kwa kongamano hilo itatangazwa wakati wowote kuanzia sasa
Kongamano hilo litazinduliwa hapa jijini na linatarajiwa kufanyika karibu nchi nzima ili kuhakikisha elimu hii ya kupambana na ajari za barabarani inaenea kote nchini

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment