JOHN JAMBELE KUMVAA MAKONGORO MAHANGA UKONGA 2010!!

Bw. John Jambele akizungumza mbele ya waandishi wa habari wakati alipokuwa akitangaza nia yake ya kugombea ubunge katika jimbo la Ukonga kweny uchaguzi ujao 2010.
Bw. John Jambele akiwa na mke wake na mtoto wao mdogo wakati alipokuwa akiongea katika mkutano na waandishi

Bwana John Jambele akizungumza na wanahabari kwenye ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati alipotangaza nia yake ya kumvaa mbunge wa jimbo la Ukonga Mh. Makongoro Mahanga Kada huyo wa CCM amewaeleza waandishi wa habari kuwa
"Mimi John Jambele napenda kuwafahamisha wanaCCM wa mjimbo la Ukonga kuwa mwaka 2010 bunge la jamhuri litakapovunjwa rasmi na majimbo yote nchini kuwa wazi, endapo mungu atanijalia uhai, afya njema nguvu na uzima mara chama cha mapinduzi kitakapotangaza mchakato wa wana CCM kuchuklua fomu za kugombea ubunge na hatimaye kuelekea kwenye kura za maoni ninatarajia kuwa mmoja kati ya wana CCM watakaochukua fomu na hatimaye kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kura za maoni kwa ajili ya kuwapa fursa wana CCM wa Jimbo la Ukonga kumpendekeza mmoja kati yetu kuwa mgombea wao kabla ya kupelekwa kwenye ngazi za juu zaidi za chama cha mapinduzi kwa ajili ya kuthibitishwa".
Jambele Ameongeza kuwa "Nimeamua kuomba kuteuliwa kugombea nafasi hii kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao 2010 kwa sababu Nia ninayo, Uwezo ninao,na Sababu za msingi ninazo, Nimesema ninao uwezo kwa sababu kwanza ni haki yangu ya kikatiba kabisa ndani ya chama cha mapinduzi na katiba ya nchi ambapo inatamkwa kwenye katiba ya CCM kuwa kila mwanachama hai wa chama cha mapinduzi mwenye akili timamu umri wa kuanzia miaka18 na kuendelea na mwenye sifa zilizoainishwa kwenye katiba anayo haki kuchagua au kuchaguliwa".

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment