Siri yafichuka Uchina

Nchini Uchina, watu takriban 60, wakiwemo waandishi wa habari kumi, wameshtakiwa kwa kuficha habari za ajali iliyotokea kwenye mgodi kwa madhumuni ya kuepuka aibu kabla ya michezo ya olimpiki ya mwaka jana.
Gazeti la China Daily linasema kwamba ajali hiyo, ambamo wachimba migodi thelathini na watatu wameuwawa, ilitokea wiki tatu kabla ya michezo ya olimpiki.
Gazeti hilo linasema maiti zilitolewa kutoka sehemu hiyo, ushahidi kuharibiwa na waandishi wa habari kupewa hongo ili kutotangaza tukio hilo.
Pia, liliongeza kwamba familia na jamaa za wachimba migodi zilishurutishwa kutokuzungumzia tukio hilo kwa vitisho na rushwa.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment