Kamishna mkuu wa jeshi la Magereza nchini, Agustino Nanyaro amesemna kwamba kesho mfungwa mwingine Bw. Semayoga Ernest kwa mara ya pili kutoka gereza la ukonga atatunukiwa shahada ya sheria na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (CKHT) , baada ya mfungwa wa kwanza Haruna Mgombela kutunukiwa shahada na chuo hicho mwaka 2007 .
Sherehe hizo zitafanyika kesho katika bustani za gereza la ukonga. Hizo zote ni juhudi za pamoja kati ya jeshi la magereza kupitia Wizara ya mambo ya ndani pamoja na wadau mbalimabli nchini katika kuwasaida wafungwa kubadili tabia wakiwa gerezani na kuhakikisha kuwa wanatoka wakiwa wema na wenye manufaa na walio tayari kujenga tiafa katika jamii zao.
Jeshi la Magereza kupitia Wizara ya Mambo ya ndani pamoja na chuo kikuu huria cha Tanzania vina mpango wa kujenga maktaba ndogo katika gereza la Ukonga pia kupita katika magerza yote nchini na kuwahamasisha wafungwa pamoja na askari magereza wajiunge na chuo hicho, yote hayo yakiwa ni kuwaelimisha na kuwatoa katika dimbwi la upungufu wa elimu, ikiwa ni kutekeleza kauli mbiu ya serikali inayosema 'maisha bora kwa kila mtanzania'.
0 comments:
Post a Comment