Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia alikuwa Mgeni rasmi Mh. Deodorous Kamala akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa ubia kati ya kampuni ya Serengeti Breweriers Ltd na East African Breweriers Ltd/DIAGEO ya Kenya katika kusambaza vinyaji vikali vinavyotengenezwa na EABL/DIAGEO hapa nchini uzinduzi huo ulifanyika jana kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jana jioni, ambapo kampuni ya Serengeti sasa inazo haki za kusambaza vinyaji vikali kutoka kapuni hiyo ya kenya hapa nchini kama vile Smirnoff,Johnnie Walker range of whiskies, Richot Brand na Bond 7.
Novemba 20/ 2009 siku ya Ijumaa jijini Arusha nchi za Afrika Mashariki zilitia saini makubaliano ya soko la pamoja kwa nchi zote zinazounda jumuiya hiyo makubaliano yanayoitwa (East Africa Community Common Market Protocol) hivyo kwa makubaliano haya ya kampuni hizi mbili kutoka Kenya na Tanzania ni mwanzo mzuri wa utekelezaji wa makubaliano hayo ya soko la pamoja kwa jumuiya yetu, kushoto katika picha ni mwenyekiti wa Serengeti Breweriers Ltd jaji Marck Bomani.
Meneja uhusiano wa Kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers Ltd Teddy Mapunda akizungumza mbele ya wageni waalikwa wakati wa uzinduzi huo.
Hapa Kocha mkuu wa timu ya Taifa Taifa Stars Marcio Maximo akiomsalimia Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana Prof. Juma Kapuya, waziri huyo ni shabiki mkubwa wa timu ya Simba na hapa ni kama vile Kocha huyo anamwambia Mh. Kapuya kuwa Hongera sana kwa mafanikio yenu wanasimba.
Kuanzia kushoto ni Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo Diodorous Kamala Waziri wa Afrika Mashariki ,Mkurugenzi wa EABL Patricia Ithau, Waziri wa anayeshughulikia Muungano Seif Maohamed Khatib na Mkurugenzi wa masoko na mauzo wa Serengeti Breweriers Shantanu Chitgopkar wakiwa wamekaa wakimsikiliza mwenyekiti wa Serengeti Breweriers Jaji Marck Bomani wakati alipokuwa akizungumza katika uzinduzi huo.
Chrristopher Mwita Gachuma Mkurugenzi wa Serengeti Breweriers Ltd Mwanza akizungumza jambo na Rais wa Shirikisho la mpira nchini TFF Rodger Tenga kulia huku Kocha mkuu wa timu ya taifa Taifa Stars Maecio Maximo katikati akipoozi kwa picha Serengeti inaidhamini timu ya Taifa na kuihudumua kwa vifaa vya michezo.
0 comments:
Post a Comment