Mchezaji Mike Chuma.
Mchezaji Soka wa Tanzania wa kimataifa wa Tanzania Mike Chuma anayecheza soka la kulipwa Nchini Denmark katika timu ya daraja la pili ya Alvarta amerejea nyumbani kwa mapumziko mafupi ya mwezi mmoja, akizungumza na FULLSHANGWE Chuma amesema amekuja nyumbani ili kutatua mambo kadhaa katika familia yake na kusalimia wazazi wake ambao wako mkoani Tanga baada ya ligi nchini humo kusimama kwa mapumziko.
Mchezaji Mike Chuma aliyekuwa akichezea katika klabu ya Valerlose amesema aliihama klabu hiyo katika majira ya baridi na kujiunga na klabu mpya ya Avarta ambayo pia iko daraja la pili.
Akizungumzaia maisha yake ya soka katika klabu hiyo mpya Chuma amesema kwa sasa bado anasaka namba kwa kuwa alikuwa majeruhi kwa muda mrefu kitu kilichopelekea kutocheza kwa muda, hata hivyo Chuma amesema kwa sasa matumaini yapo katika timu yake mpya ya Avarta ambapo mchezaji mwenzie ambaye wanacheza namba moja Philip Jasper anayechezea pia timu ya taifa ya vijana ya Denmark anatarajiwa kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka nchini Uturuki hivyo kama atafanikiwa katika majaribio yake yeye atakuwa amejinyakulia namba katika klabu hiyo ya Avarta
Mike Chuma aliyewahi kuichezea timu ya Simba kabla ya kwenda Denmark amesema anatarajia kurejea nchini nchini humo ili kuendelea na kibarua chake katika timu yake mpya baada ya wiki moja ijayo.
1 comments:
tunaomba ututafutie kama kweli danmark kuna timu hiyo, maana najua ni muongo huyoau wewe mjengwa sahihisha maana unaharibiwa blog na waongo waongo hao.Danmark hakuna timu hiyo daaja la pili labda la saba
Post a Comment