MANJU MSITA NA UBUNIFU WA MAVAZI YA KIAFRIKA!!

Manju Msita mbunifu wa mavazi aliyeshiriki katika maonyesho ya Swahili Fashion Week yaliyomalizika hivi karibuni katika Viwanja vya Karimjee akipita mbele ya wageni waalikwa mara baada ya wanamitindo kupita jukwaani na mavazi yake aliyobuni, baada ya shughuli hiyo kubwa FULLSHANGWE imeongea na mbunifu huyo mahiri nchini na anasema "Nilizaliwa ili nibuni kwani nilipokuwa tumboni mwa mama yangu ndipo hasa nilipokuwa shule, na siku nilipozaliwa ndipo nilipotunukiwa Shahada yangu ya ubunifu"
Kwa kifupi ni kwamba kuna mambo unayakuta duniani na kuna mambo mengine unakuja nayo duniani, kwa suala la ubunifu ni lazima uje nao kwani ni hakuna mtu atakufundisha kubuni na kama itatokea kufundishwa basi utajifunza yale aliyonayo yeye.
Hebu angalia ubunifu huu wa mbunifu Manju Msita uweze kuona kazi zake na uwezo wake katika kubuni mavazi kazi kwako Mdau wa FULLSHANGWE.

Umewahi kuona Mvuvi akiwa ameongozana na samaki hebu angalia ubunifu huu wa Manju Msita ulivyosheheni vitu.

Kumbe gunia likichanganywa na Linen linaweza kumtoa mwanamke bomba kama hivi.

Unaonaje Linen inapochanganywa na gunia unapata picha?
Hii ni ya kiume na imechanganywa kwa kitambaa cha Linen iliyochanagnywa na Kitenge.
Hii nguo imetengenezwa kwa bridal satin na kitenge kama unavyoiona inapendeza ukiitazama.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment