KAZI YA HESHIMA YA MWANAMUZIKI YOUSSOUR NDOUR!!

Mwanamuziki Youssou Ndour anayeheshimika sana duniani kutoka nchini Senegal akiimba mbele ya mashabiki lukuki waliohudhuria katika onyesho lake pamoja na mwanamuziki wa kike kutoka Benin Angelique Kidjo wakati wa tamasha la muziki la taasisi ya Mohamed Mo lililofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam usiku wa kuakia leo onyesho hilo limekuwa ni changamoto kwa wanamuziki wa hapa nyumbani na afrika pia kwani mwanamuziki huyu amekuwa akitumia vifaa vya kiafrika kama vile Talkingdrum, percussion (ngoma za asili) pamoja na vifaa vingine vya kisasa ambavyo vimekuwa vikitengeneza muziki wenye ladha na midundo halisi ya kiafrika inayokubalika sehemu yoyote duniani na ndiyo maana amekuwa akipata heshima kubwa duniani na hii inadhihirisha kuwa kumbe kuna muziki mwingine mzuri zaidi hata ya muziki wa bolingo kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo
Hapa Youssou Ndour akiimba kabla mashabiki hawajaanza kupandisha mzuka
Mwanamuziki Anjelique Kidjo akifanya vitu vyake kwenye tamasha la muziki la Ibrahim Mo lililofanyika jana kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment