MAKAMPUNI 15 YATOA MSAADA KWA JESHI LA POLISI!!

Waziri wa mambo ya Ndani Lawrence Masha kushoto pamoja na Inspekta Generali wa Polisi Saidi Mwema wakisikiliza jambo wakati wa makabidhiano ya vifaa mbalimbali vya utendaji kazi kwa jeshi la polisi Dar es Salaam, msaada ni kutoka katika makampuni mbalimbali nchini.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na buti 500, kofia za barret 1000, viatu vya kawaida jozi 200, seti moja ya jezi za mpira wa miguu, seti 1 ya jacketi za riadha, cardon tape mita 10,000, vitabu 400 vya kurekodi taarifa za uhalifu, mikanda ya filimbi 500, gloves 500, key holders 300, reflector 500, stable belt 500, mobile hand set 10 na solar lamp vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni mia moja kumi na nne, laki sita na thelathini.
Makampuni yaliyotoa vifaa hivyo ni pamoja na Italy Shoes Co Ltd, JM Tredars, Regalia Tanzania ltd, Katwe International Co ltd, Chama cha Riadha Tanzania, Cozy Tredars, Lugumi Interprise Ltd, Digital international, Dry Cell General traders, Open Sanity, Status Investiment, BigBon Petroleum Ltd, Mhonyiwa and Company ltd,Daissy General Traders

Picha ya pamoja ya wawakilishi wa makampuni, waziri Masha na wawakilishi wa jeshi la polisi.


You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. Hivi jamani kwanini jeshi linapewa misaada? Ikitokea mtoa misaada amekosa hili jeshi litaweza kumkamata kweli?

Post a Comment