Timu ya Yanga ya jijini Dar es salaam leo imejiweka katika mazingira mazuri kwenye msimamo wa ligi kuu ya Vodacom iliyondelea kwenye uwanja wa Uhuru wakati ilipomenyana na watoto wa mji kasoro bahari Moro United
Yanga ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata goli katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo baada ya mchezaji wake Nurdin Bakari kuwazidi ujanja mabeki wa timu hiyo na kuubetua mpira juu mbele ya golikipa wa Moro United hivyo kuandika goli hilo lililowafanya kuongoza mpaka kipindi chote cha kwanza kilipomalizika.
Katika kipindi cha pili cha mchezo huo Moro United walionekana kuelewana vyema na kujipanga kwa mashambulizi ya mara kwa mara katika ngome ya yanga, hata hivyo washambuliaji wa timu hiyo hawakuwa makini kitu kilichowafanya washindwe hata kupata goli moja mbele ya vijana hao wa mtaa wa Jangwani kitu kilichoifanya Yanga kuibuka na ushindi wa goli 1-0 na kufikisha pointi 18
Mchezo wa leo uanawaweka yanga katika nafasi nzuri kwa morari wakati watakapopambana na watani wao wa jadi timu ya Simba ya jijini Mchezo wa ligi kuu ya Vodacom unaotarajiwa kupigwa kwenye uwanja mkuu wa Taifa oktoba 31 siku ya Jumamosi, Timu ya Simba mara baada ya kumaliza mchezo wao wa jana dhidi ya Azam Fc ilirejea tena mjini Zanzibar ambako imepiga kambi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo

0 comments:
Post a Comment