SWAHILI FASHION WEEK YAZINDULIWA RASMI, KUFANYIKA JIJINI DAR NOV 4-6-09!!

Mustafa Hassanali akizungumza wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya mavazi ya Swahili Fashion week uliofanyika jana kwenye ukumbi wa Runway pale Shoperz Plazza, maonyesho hayo yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujaoa hapa jijini Dar es salaam kwenye ukumbi wa Karimjee kuazia Novemba 4- 6 mwaka huu.
Mustafa Hassanali amesema maonyesho hayo yatashirikisha wabunifu wa mavazi kutoka hapa nchini wapatao 13 wakati wengine wawili wakitoka nchini Kenya na Mmoja akitoka nchini Uganda huku wengine wakitoka katika nchi za Afrika Kusini na Msumbiji
Mustafa ameongeza kuwa maonyesho hayo yataleta sura mpya hapa nchini kwa upande wa wabunifu wa mavazi kutokana na kwamba watashiriki wabunifu wengine kutoka nje ya Tanzania hivyo itakuwa ni nafasi pekee kwa wabunifu wetu hapa nchini kubadilishana utaalamu wa kubuni mavazi huku wakiongeza mawasiliano kutokana na wageni mbalimbali watakaotembelea katika maonyesho hayo.
Mustafa Hassanali akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Mwamvita Makamba

MwanamuzikiBanana Zorro wa B. Band akitumbuiza wakati wa uzinduzi wa maonyeshop ya mavazi ya Swahili Fashion week yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujaoa katika ukumbi wa Karimjee.

Kutoka kulia ni Doreen,Stella Sakia na Grolly Mungure kutoka Infinity wakiwa katika pozi

Gardiner G Habash akiwa na Maiwaifu wake Lady JayDee wa Machozi Band.

Rajab Mchatta wa Big Solution na maiwaifu wake nao wakawakilisha.

Mustafa Hassanali katikati akiwa na wadau wa mitindo.


Jaquiline Ntuyabaliwe aka Kylin kushoto na Mercy Galabawa.

Wadu hawa pia walikuwepo.

Ancle Albert Makoye mkuu Itifaki Miss Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na Mbunifu wa mavazi Farha.

Kisa kushoto na Mange waliwakilisha pia

Wabunifu wa mavazi kutoka kulia ni Zamda George, Khadija Mwanamboka na Farha.

Wanamituimndo mbalimbali walihudhuria katika uzinduzi huo.

Wageni kutoka makampuni mbalimbali walialikwa katika uzinduzi wa Swahili Fashion Week jana jioni.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

2 comments:

  1. Jamani kivazi cha JD ni balaa. au mnasemaje wadau. kazi kweli kweli

  2. KILA MARA ANAYEIGA HUPITILIZA KULIKO YULE MWENYE TABIA.

Post a Comment