Wanyama wanateswa sana kabla ya kuchinjwa na kufanywa kitoweo hebu cheki Mbuzi huyu!!

Zakaria Owindo mkazi wa Butiama wilayani Musoma katika mkoa wa Mara akiwa amembeba mbuzi katika baiskeli kutokea kijiji cha Kyabakari kwa ajili ya kumchinja na kuuza nyama choma wakati wa maonyesho ya wiki ya vijana yaliyomalizika hivi karibuni kijijini hapo. Wananchi wengi waliweza kufanya biashara mbalimbali wakati wa maonyesho hayo na kujipatia kipato. Kwa siku wafanyabiashara wa nyama choma walikweza kuuza mbuzi wa tatu hadi wanne kwani nyama hiyo ilikuwa inauzwa kuanzia Tshs.1000/= na kuendelea.


You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment