MKALI JOSSE MARA ANAVYOFANYA MAMBO FM ACADEMIA!!

Josse Mara mwanamuziki Pekee mtanzania anayetamba katika Bendi ya muziki ya FM Academia watoto wa Mujini kutokana na uwezo wake katika kuimba na kutawala jukwaa, watu wengi wamekuwa hawaamini kama kweli mwanamuziki huyu ni mtanzania lakini ukweli ndiyo huo, jamaa anakamua kisawasawa sambamba na wanamuziki wenzie wa bendi hiyo yenye wanamuziki wengi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,
Pamoja na Bendi hiyo Kukubalika na mashabiki kutokana na uwezo wao katika kupiga muziki lakini pia Josse Mara amechangia kwa kiwango kikubwa bendi hiyo kukubalika na watanzania wengi kwani yeye ndiye anayebeba utanzania halisi katika bendi hiyo hivyo anastahili kupongezwa kutokana na uwezo wake lakini pia kufanya kazi na wenzake kwa ufanisi mkubwa katika bendi hiyo, usiku wa kuamkia leo Camera ya FULLSHANGWE baada ya kutoka kwenye uzinduzi wa Swahili Fashion week ilijimuvuzisha mpaka kule Equator Grill Mtoni na kuwafuma jamaa wakikamua vilivyo huku vimwana wa bendi hiyo wakitakatisha jukwaa kitu kilichomfanya kamanda mshika Camera wa FULLSHANGWE aahirishe zoezi la kuwapotezea wakali hao wa muziki wa Bongo na kuanza kufyatua picha mbalimbali za matukio katika onyesho hilo.
Palikuwa hapatoshi wakati Pablo Masai alipokuwa akioongoza mashambulizi jukwaani huku vimwana wa bendi hiyo wakionyesha jinsi wanavyoweza kuzungusha viuno hebu wacheki mdau.

Hapa kazi ni moja tu hata kama hupendi kwenda kucheza utaenda tu wala hutashikiwa bastola utaenda mwenyewe



You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment