Rais Kikwete aweka jiwe la msingi kituo cha Watoto yatima Rungwe!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Lucy Hope Centre Bi.Lucy Mwandosya pamoja na Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya muda mfupi baada ya kuwahutubia wananchi wa Lufilyo,Rungwe wakati wa uwekaji jiwe la Msingi katika jingo la taasisi hiyo uliofanyika jana.Taasisi ya lucy Hope inawahudumia watoto Yatima.(picha na Freddy Maro).

Rais Jakaya Mrisho Kikwete,mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Lucy Hope Centre Bi.Lucy Mwandosya na Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya wakishangalia wakati wa hafla ya kuweka jiwe la Msingi katika jingo la taasisi hiyo iliyofanyika huko Lufilyo,Rungwe, mkoani Mbeya jana jioni.Taasisi ya Lucy Hope inawahudumia watoto Yatima kwa kuwalea na kuwapa elikmu katika ngazi mbalimbali

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Lucy Hope Centre Bi.Lucy Mwandosya na Mumwewe Profesa Mark Mwandosya wakimkabidhi picha iliyochorwa na Bi.Lucy mwandosya inayoonesha ngoma ya utamaduni ya Rungwe wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la taasisi hiyo huko Lufilyo Rungwe jana jioni.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment