Mwenge wa Mwitongo wawashwa kumkumbuka Mwalimu J.K.Nyerere!!

Mama Maria Nyerere akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa kiongozi wa mbio hizo kitaifa Kheri Ahmada Mwawalo kutoka mkoa wa mjini Magharibi mara baada ya mwege huo kuwasili nyumbani kwake kijijini Butiama wilayani Musoma katika mkoa wa Mara kwa ajili ya kuuwasha mwenge wa Mwitongo. Tangu kuwashwa kwa mwenge wa Uhuru mwaka 1961, mwenge wa Mwitongo uliopo nyumbani kwa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere huwa unawashwa kila mwaka na unajizima wenyewe baada ya mafuta kuisha. Mwenge huo unatarajiwa kuzimwa kesho kijijini Butiama huku siku hiyo ikiwa ni maadhimisho ya miaka kumi tangu kufa kwa Baba wa Taifa
Mwenge wa Mwitongo uliopo nyumbani kwa hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kijijini cha Butiama wilayani Musoma mkoa wa Mara ukiwa unawaka mara baada ya kuwashwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Kheri Ahmada Mwawalo . Tangu kuwashwa kwa mwenge wa Uhuru mwaka 1961, mwenge wa Mwitongo huwa unawashwa kila mwaka na unajizima wenyewe baada ya mafuta kuisha.
Picha Na Anna Nkinda - Maelezo

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Kheri Ahmada Mwawalo kutoka mkoa wa mjini Magharibi akiuwasha mwenge wa Mwitongo uliopo nyumbani kwa hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kijijini cha Butiama wilayani Musoma mkoa wa Mara . Tangu kuwashwa kwa mwenge wa Uhuru mwaka 1961, mwenge wa Mwitongo huwa unawashwa kila mwaka na unajizima wenyewe baada ya mafuta kuisha.

Wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka 2009 wakiomba dua katika kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lililopo kijiji cha Butiama wilayani Musoma mkoa wa Mara.


You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment