
Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Rais kuwasili katika uwanja wa ndege wa Musoma jana jioni.Rais Kikwete yupo mkoani Mara kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo pamoja na shughuli nyingine atakuwa mgeni rasmi katika kilele cha mbio za mwenge.(picha na Freddy Maro)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kitufe wakati akizindua mradi wa umeme katika kijiji cha Kisamwene kata ya Butuguri,wilaya ya Musoma vijijijni jana jioni.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mwanafunzi Ezekiel James wakati alipokagua darasa la mfano muda mfupi baada ya kufungua shule ya Sekondari ya Chifu Oswalds Mang’ombe jana wilaya ya Musoma vijijini

Mwanafunzi Godbless Buluhya wa shule mpya ya sekondari ya Chifu Oswalkd Man’gombe iliyopo musoma vijijini akifanya jaribio la kisayansi wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete(Watatu kulia) alipokagua maabara ya shule hiyo jana jioni.Wengine katika
kutoka kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Mstaafu Enos Mfuru(wapiloi kushoto) na wane kuli ni Mbunge wa Musoma vijijini Nimrod Mkono
0 comments:
Post a Comment