Na shaaban MpaluleMawakala wa Mikoa na Wilaya Miss Utalii Tanzania 2009 wametangaza ratiba ya Mashindano ya Miss Utalii katika maeneo mbalimbali ikiwa ni katika kuelekea Fainal za Taifa zilizopangwa kufanyika mwezi Disemba mwaka huu, Katika ratiba hiyo ni mikoa michache tu ambayo haikuweza kuwasilisha tarehe ya mashindano ambapo mawakala wa Wilaya wametakiwa kuwa wamekamilisha zoezi hilo kabla ya tarehe 15 mwezi wa 11 ili kutoa nafasi kwa Waandajii wa Kanda ambao wanatakiwa kukamilisha zoezi hilo kabla ya Disemba 1 mwaka huu.
Kwa Upande wa Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam Ilala wao watashindana tarehe 30 katika Ukumbi wa Da’ West Tabata mwezi huu, Kinondoni watashindana tarehe 7, mwezi wa 11 katika Ukumbi wa New Msasani Klabu, na washindi wa Wilaya zote za Dar es Salaam watashindana tarehe 21 mwezi wa 11.Mkoa wa Kilimanjaro wao watashindana tarehe 31 mwezi huu, wakati Mkoa wa Iringa wenyewe wamepanga kushindana tarehe 6 mwezi wa 11, na Kagera Wenyewe wamepanga kushindana tarehe 13 mwezi wa 11, wakati Mtwara wanatarajia kumenyana tarehe 20 mwezi wa 11.
Akizungumzia shindano hilo Rais wa Miss Utalii Tanzania Gideon Chipungahelo alisema kuwa Mikoa mingine bado wanaendelea na mikakati ya kufanikisha shindano hilo lakini hata baadhi ya Mikoa tayari wamekwisha kamilisha zoezi hilo .Aidha Chipungahelo aliwataka baadhi ya Warembo kujitokeza katika Mikoa yao kushirikin Shindano hilio ambalo kwa mwaka huu limeonyesha kuwa na mafanikio makubwa ikilinganishwa na miaka ya nyuma.“nchi yetu tunao warembo wengi wenye sifa nyingi za kushiriki, lakini wanashindwa kujitokeza, isipokuwa nachukua fulsa hii kuwatangazia kwamba, wakatin umefika wa wao kujitoa ili kuhakikisha wanaipeperusha bendera ya nchi yao, wasikae tu majumbani wakati wao wanastaili kuwa mabalozi wema katika kuutangaza utalii wan chi, na kwa kuwa bado nafasi zipo, wajitokeze ili waweze kushiriki, kwani hii ndiyo nafasi kwao, “alisema Chips





0 comments:
Post a Comment