Milioni 31 zapatikana katika Harambee ya kuchangia Ujenzi wa shule ya Agape!!

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.

Na Anna Nkinda - Maelezo, aliyekuwa Morogoro
24/10/2009 Jumla ya shilingi milioni 31 zimepatikana katika Harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya Msingi ya Agape ya Kanisa la Waadiventista Wasabato iliyopo mkoani Morogoro.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ndiye aliyekuwa mgeni rasmi kwenye Harambee hiyo iliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Hoteli ya Morogoro.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) aliwataka wadau mbalimbali wa elimu waliohudhuria katika harambee hiyo kutoa kwa moyo kadri Mwenyezi Mungu alivyowajalia kwani Mungu aliyewapa ndiye wanayemtolea kwa njia ya ujenzi wa shule ambayo itawasaidia watoto kukua katika malezi yanampendeza Mungu.
"Napenda kuwapongeza wote waliotoa wazo la kufanya shughuli ya kuchangia ujenzi wa shule ya Agape kwani ujenzi wa shule hii ni wa muhimu sana kwakuwa utaongeza fursa ya watoto kupata elimu bora na malezi mazuri", alisema Mama Kikwete.
Akisoma taarifa ya shule hiyo Levi Yango ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule alisema kuwa ujenzi wa shule hiyo ambayo ni ya mchepuo wa kiingereza ulianza tangu mwaka 2003 huko Kitungwa umbali wa kilomita 12 kutoka Morogoro mjini.
Kabla ya kuanza kwa ujenzi wa shule hiyo wanafunzi wa darasa la kwanza walianza mwaka 2002 katika eneo la kanisa ambako kulikuwa na majengo ya vyumba vinne vya madarasa, vyoo matundu saba na ofisi moja ya walimuAliendelea kusema kuwa kutokana na ushauri wa Mkaguzi Mkuu wa Elimu Manispaa ya Morogoro walilazimika kutafuta eneo lingine huko Kitungwa na kuanza ujenzi ambako kanisa limeshakamilisha ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na vingine vitatu vipo katika hatua ya ukamilishaji.
Yango alisema, "Kwasasa shule imekuwa ikitumia majengo yasiyo rasmi yaliyopo karibu na shule kwa baadhi ya shughuli zingine kama vile ofisi ya walimu, vyumba kwa ajili ya darasa la kwanaza na la pili majengo mbayo hayakidhi mahitaji kitaaluma".
"Hali hii imechelewesha usajili wa kudumu ili kupata usajili wa kudumu , Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (Idara ya Ukaguzi) imeshauri tukamilishe ujenzi wa vyumba vitatu vilivyobaki na jengo la utawala lenye ofisi za walimu".

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. Agape na bendera za ccm kuna uhusiano gani?

Post a Comment