Warembo watakaoiwakilisha Nchi ya Rwanda katika mashindano ya kimataifa ya MISS EAST AFRICA 2009 watapatikana wiki hii katika mashindano yanayosubiliwa kwa hamu kubwa Nchini humo.
Mashindano hayo ya Rwanda yanaayoandaliwa na kampuni ya Rwanda Events Limited ya Nchini humo yatafanyika siku ya Jumamosi wiki hii jijini Kigali.
Washindi wawili wa mashindano hayo wataiwakilisha Nchi ya Rwanda katika fainali za mashindano ya MISS EAST AFRICA 2009 yatakayofanyika tarehe 18 Desemba, 2009 jijini Dar es salaam, Tanzania.
Wawakilishi wa Rwanda katika mashindano ya Miss East Africa mwaka jana yaliyofanyika Bujumbura, Burundi walikuwa ni Kaneza Brigitte na Idmulisa Dominique from RWANDA
Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu yanatarajiwa kushirikisha warembo 28 kutoka Nchi 14 ambazo ni pamoja na wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, na Burundi. Zingine ni Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Somalia, Madagascar, Seychelles, Mauritius, Comoros, na Re union,
Mashindano ya Kimataifa ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Limited ya jijini Dar es salaam.
Wakati huohuo droo ya kila mwezi ya bahati nasibu ya Miss East Africa imefanyika jana na washindi kutangazwa. Washindi hao wa droo ndogondogo za kila mwezi wamejishindia zawadi mbalimbali zenye thamani ya shillingi million mbili ikiwa ni pamoja na pesa taslimu, simu za mkononi, ticketi za VIP za kuangalia fainali ya mashindano ya Miss East Africa, n.k.
Zawadi kubwa katika bahati nasibu hiyo inayoendelea Nchi nzima ni Gari aina ya Range Rover Sport, kutoka CMC Automobile Ltd. Ili kushiriki bahati nasibu hiyo unatakiwa kununua ticketi kutoka kwa wauzaji wa Magazeti Nchini, au kutuma SMS ya neno “SHINDA” kwenda namba 15567 kwa kutumia simu ya mkononi.
0 comments:
Post a Comment