
Mama Maria Nyerere (aliyevaa nguo ya kijani) akiiangalia zawadi ya picha ya Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyopewa na bodi ya Makumbusho ya Taifa . Picha hiyo ni moja ya vionyesho vilivyotayarishwa na bodi hiyo wakati wa maonyesho ya wiki ya vijana yanayomalizika leo kijijini Butiama katika wilaya ya Musoma mkoani Mara. Kilele cha maadhimisho ya wiki hiyo kitakwenda sambamba na sherehe za kuzimwa kwa Mwenge wa Uhuru pamoja na kumbukumbu ya miaka kumi tangu kufa kwa Baba wa Taifa zitakazofanyika katika kijiji hicho.
Wasanii wa Kikundi cha Waelimishaji rika Jamii kata ya Kiriba (KIWAJAKI) wakicheza ngoma ya Munenguro ya kabila la Waruli. Kikundi hicho kilikuwa kinawaburudisha wananchi wa kijiji cha Butiama kilichopo wilayani Musoma mkoani Mara wakati Mwenge wa Uhuru ulipowasili katika kijiji hicho jana kwa ajili ya kuuwasha mwenge wa Mwitongo.Mwenge huo unatarajiwa kuzimwa leo katika kijiji hicho huku ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya miaka kumi tangu kufa kwa Baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
0 comments:
Post a Comment