Noel Tenga mkurugenzi wa Christian Directory and Consultancy (T) akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi zake zilizopo magomeni kulia ni mwimbaji Upendo Kilahiro.
Upendo Kilahiro akiimba katika moja ya maonyesho yake.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Fredriki Sumaye, anatarajiwa kuongoza maelfu ya watu katika tamasha kubwa la kuchangia taasisi ya Saratani ya Ocean Road litakalofanyika Mkoani Arusha hivi karibuni.
Tamasha hilo ambalo linatarajiwa kuwa la aina yake kuwahi kufanyika katika Mkoa huo wa Arusha, litafanyika Jumapili ya tarehe 8 Novemba 2009, katika Uwanja wa Karume.
Tamasha hilo la kihistoria linakwenda sanjari na kutambulishwa rasmi kwa albamu ya muziki wa Injili inayoitwa ‘Asante Yesu’ ya mwimbaji Upendo na Amon Kilahiro.
Uzinduzi wa albamu hii ya ‘Asante Yesu’ ya Upendo Kilahiro umekuja mara baada ya kupita kipindi cha takribani miaka mitatu tangu afanye tamasha kama hilo katika Mkoa huo wa Arusha wenye sifa ya kuwa na watalii wengi.
Baada ya kuwa katika safari za Injili katika nchi nyingi kama vile Afrika Kusini, Canada na Marekani sasa mwimbaji huyo amerudi nyumbani kuja kumtukuza Mungu.
Tamasha hili la kusifu na kuabudu pamoja na uzinduzi wa ‘Asante Yesu linasimamiwa na kuandaliwa na taasisi ya Christian Directory and Consultancy (T) kwa kushirikiana na Upendo na Amon Kilahiro.
Akizungumza na waandishi wa habari, msemaji wa taasisi ya Christian Directory and Consultancy(T), Bwana Noel Tenga alisema kuwa lengo kubwa la tamasha hilo ni kukusanya fedha za kufanya kampeni ya kusidia watu wenye uhitaji. Kampeni ambayo itakuwa ni ya kudumu na kwa sasa wamelenga kusaidia watua wagonjwa wa Saratani.
“Katika tamasha letu hili tuna lengo la kukusanya fedha ambazo sehemu kubwa itakwenda kusaidia wagonjwa wa Saratani katika taasisi ya Ocean Road.
“Tutazindua rasmi kampeni ya kusaidia watu wenye uhitaji, kwa safari hii tumekusudia kwenda kutoa msaada katika taasisi ya Ocean Road, hasa katika eneo la kununua mashine ya kuchujia maji na kukarabati sehemu ya majengo ya wodi ya wagonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi,” alisema Noel Tenga.
Aidha msemaji huyo alisema, tamasha hilo pia linatarajiwa kudhuriwa na watu mbalimbali wa kada tofauti tofauti, na kwamba mgeni rasmi wa tamasha hilo atakuwa Mh. Fredriki Sumaye, ambaye atasindikizwa na wageni wengine waalikwa ambao ni wabunge na wafanyabiashara mbalimbali kutoka katika Mkoa huo wa Arusha
Katika tamasha hilo mwimbaji Upendo na Amon Kilahiro wanatarajiwa kuimba nyimbo zote katika albamu hiyo ya Asante Yesu ‘live’ na si kama ilivyozoeleka katika matamasha mengine.
Tamasha hili litapambwa na waimbaji wengine wa nyimbo za injili hapa nchini ambao ni Christina Shusho, Jenifer Mgendi, Victor Aaron, JoJo Jose na mke wake Matlida Mlay na waimbaji wengine wengi.

0 comments:
Post a Comment