TENGA AWAFAGILIA WACHEZAJI WA KULIPWA SIMBA, ASEMA WANASTAHILI KUITWA WACHEZAJI WA KULIPWA!!

Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Reodger Chila Tenge.

Rais wa Shirikisho la soka nchini TFF Bw. Reodiger Tenga amewasifu wachezaji wa kulipwa wa simba kutokana na uwezo mkubwa na nidhamu ambayo wachezaji hao wamekuwa wakionyesha mara kwa mara katika michezo mbalimbali ya ligi kuu ya Vodacom ambayo wamekwa wakishiriki na Timu yao.
Tenga ameyasema hayo leo mbele ya waandishi wa habari wakati wa mdahalo uliokuwa umeitishwa kati ya Rais huyo na chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA katika makao makuu ya shirikisho hilo pale Karume ili kujadili mambo kadhaa juu ya mstakabali wa soka letu
Mdahalo huo ulikuwa ni wa kujadili hatua mbalimbali ambazo shirikisho la soka TFF limechukua dhidi ya waamuzi wanaovurunda katika uchezeshaji wao na kupelekea baadhi ya waamuzi kufungiwa maisha na kutojishirikisha na shughuli zozote za mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini, kuna waamuzi kadhaa wamefungiwa na shirikisho hilo wakiongozwa na bosi wao mwamuzi wa kati Othman Kazi
Rais huyo wa TFF aliwaelezea wachezaji Hirary Echesa, Emmanul Okwi na Joseph Owino wote wa Simba kuwa ni wachezaji mahiri na wanaostahili kuitwa wachezaji wa kulipwa kutokana na uwezo ambao wameonyesha katika michezo mbalimbali waliyocheza na kuonyesha kiwango cha hali ya juu kinidhamu, hivyo akasema wachezaji hao wanastahili kupongezwa kwa wanachokifanya na kwamba ni wachezaji wenye kuleta changamoto kubwa kwa wachezaji wetu wa ndani lakini pia kwa wachezaji wengine wa kulipwa wanaochezea timu za hapa nyumbani.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment